Ijumaa, 20 Oktoba 2017

WAKALA WA SEREKALI WA HUDUMA ZA MATREKTA NA ZANA ZA KILIMO WATIA FORA MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

 Mkurugenzi wa Wakala wa Serekali wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo Nd. Affan Othman Maalim akitoa maelezo kwa Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea banda la wakala kwenye maonyesho ya siku ya chakula Dunia, akitoa maelezo jinsi ya sehemu ya machine shop inavyofanya kazi zake na kumuhakikishia kuwa wakala wamejipanga kwa kila sekta kwa kutumia wataalam wake kwa kutoa hududma bora.

 pia alitembelea kitengo cha ukarabati cha wakala na kuonyeshwa zana mbali mbali za kilimo ambazo husimamiwa na wakala na kutoa huduma nzuri kwa wakulima wa Unguja na Pemba na kuhakikisha ukulima unafanikiwa.

Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akilagua mashine ya kuvunia mpunga kwenye Maonyesho ya siku ya chakula Duniani yaliyofanyika Dole.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni